Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika hifadhi kubwa ya wanyama karibu na mji waliishi wanyama wengi wa aina tofauti. Kulikuwa na Tembo mkubwa aliyeitwa Kito na Sungura mdogo aliyeitwa Pili.
Kito alikuwa mwenye nguvu sana lakini wakati mwingine alijivunia nguvu zake. Pili alikuwa mdogo lakini alikuwa na akili nyingi.
Siku moja kulikuwa na ukame. Maji yakapungua sana kwenye bwawa la wanyama. Wanyama wote wakaanza kuwa na wasiwasi.
“Tutakunywa wapi maji?” swali hilo liliwafanya wote kuwa kimya.
Kito akasema kwa sauti kubwa “Mimi ni mkubwa na mwenye nguvu. Nitayachimba maji peke yangu!”Akaanza kuchimba kwa nguvu sana. Lakini alichoka haraka na maji hayakutoka.
Pili akamwambia kwa upole “Kito labda tukishirikiana wote tunaweza kufanikiwa.”
Mwanzoni Kito hakupenda wazo hilo. Lakini baada ya kufikiria alikubali. Wanyama wote pundamilia, swala tumbili na hata ndege wakaanza kusaidiana.
Baada ya muda wakafanikiwa kuchimba sehemu yenye maji safi. Wanyama wote wakashangilia kwa furaha. Kito akamgeukia Pili na kusema
“Leo nimejifunza kuwa nguvu peke yake haitoshi. Ushirikiano ni muhimu.”
Pili akatabasamu “Ndiyo hata mdogo anaweza kuwa na mchango mkubwa.”
Tangu siku hiyo wanyama waliishi kwa kusaidiana na kuheshimiana.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Post a Comment