Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mtoto mmoja aliyeitwa Neema alikuwa msichana mdadisi sana. Alipenda kuuliza maswali na kugundua mambo mapya kila siku.
Siku moja akiwa njiani kwenda shule aliona pochi ndogo chini ya mti. Aliichukua na kufungua kidogo. Ndani kulikuwa na pesa na kitambulisho cha mtu mzima aliyeitwa Bwana Juma.
Neema alijiuliza “Nifanye nini sasa?”
Rafiki yake Asha akasema “Labda tuzipeleke dukani tununue peremende.”
Lakini Neema akatikisa kichwa. “Hapana si zetu. Lazima tumrudishie mwenyewe.”
Baada ya shule Neema alienda kwa mwalimu wake na kumwonesha ile pochi. Mwalimu alifurahi sana na kusema “Umefanya jambo la uaminifu. Twende tukamtafute mwenyewe.”
Walifuata anwani iliyokuwa kwenye kitambulisho na kufika nyumbani kwa Bwana Juma. Alipowaona alikuwa na wasiwasi sana kwa sababu alikuwa amepoteza pochi yake asubuhi ileile.
Neema alimkabidhi pochi yake. Bwana Juma alifurahi mno. “Asante sana mwanangu. Umeonyesha uaminifu mkubwa.”
Alitaka kumpa Neema zawadi ya pesa lakini Neema akasema kwa upole “Asante lakini nilifanya kwa sababu ni jambo sahihi kufanya.”
Tangu siku hiyo watu wa kijiji walimjua Neema kama mtoto mwaminifu. Na Neema alijifunza kuwa kufanya jambo sahihi huleta furaha moyoni kuliko zawadi yoyote.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment