Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Hapo zamani za kale katika kijiji kidogo kilichokuwa karibu na mto waliishi watoto wawili waliokuwa marafiki sana. Majina yao yalikuwa Amani na Rehema. Kila siku walicheza pamoja baada ya kutoka shule.
Siku moja waliona ndege mdogo ameanguka kutoka kwenye mti. Ndege huyo alikuwa akitetemeka kwa hofu. Amani alisema
“Tumsaidie ameumia.”Rehema alikubali na kwa upole wakambeba yule ndege na kumhuendaweka kwenye kikapu chenye majani laini. Walimpatia maji kidogo na nafaka. Kila siku walimhudumia kwa upendo.
Baada ya siku chache ndege yule alipona. Siku moja asubuhi aliruka juu na kuzunguka hewani kana kwamba anawaaga. Amani na Rehema walifurahi sana kuona amepona.
Mama yao aliwaambia“Mtoto mwema hujulikana kwa matendo yake. Mungu hupenda watoto wenye moyo wa hur uma.”
Watoto walijifunza kwamba kusaidia wengine ni jambo jema na huleta furaha moyoni.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment