MATENDO MEMA YANAWEZA KUFUNGUA MILANGO YA BARAKA

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Hapo zamani kidogo katika jiji la Mwanza aliishi mvulana mmoja aitwaye Tino. Tino alipenda sana magari na ndoto yake ilikuwa kuwa dereva wa basi kubwa siku moja.

Kila jioni baada ya shule Tino alimsaidia mama yake kuuza matunda pembeni ya barabara. Siku moja kulikuwa na mvua kubwa na watu wengi walikuwa wanakimbia kujikinga. Katika haraka hiyo mzee mmoja alisahau begi lake kwenye benchi karibu na kibanda chao.

Tino aliliona lile begi. Alipolifungua kidogo akaona kulikuwa na nyaraka muhimu na pesa.

“Mama kuna begi limeachwa hapa ” Tino alisema Mama yake akamwambia “Tusilichukue. Mwenyewe atalirudia au atalitamani sana.”

Baada ya dakika chache mzee yule alirudi akiwa na wasiwasi mkubwa.

“Jamani kuna mtu ameona begi langu?” aliuliza Tino akasimama haraka “Ndiyo babu hili hapa.”

Mzee yule alifurahi sana. Alisema, “Humu kuna vyeti vyangu na pesa ya kodi ya nyumba. Asante sana mwanangu.”

Siku chache baadaye yule mzee alirudi tena. Kumbe alikuwa mmiliki wa kampuni ndogo ya usafiri mjini. Alimwambia Tino “Kwa sababu ya uaminifu wako nitakuruhusu uje mara moja moja ujifunze kuhusu magari kwenye gereji yangu.”

Tino aliruka kwa furaha ndoto yake ilianza kutimia kwa sababu tu alichagua kuwa mwaminifu.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments