Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mtoto aitwaye Neema. Neema alikuwa msichana mwerevu lakini alikuwa na tabia moja mbaya aliogopa kusema ukweli alipokosea.
Siku moja alipokuwa akicheza ndani ya nyumba alivunja kikombe cha mama yake. Alishtuka sana. Akaamua kukificha chini ya kitanda.
Mama aliporudi aliona kikombe hakipo. Akauliza “Neema unajua kilipo kikombe changu?”
Neema akahisi moyo wake ukidunda kwa kasi. Alitaka kusema hajui lakini akakumbuka maneno ya mwalimu wake: “Ukweli ni kama taa huondoa giza.”
Kwa sauti ya chini akasema “Samahani mama mimi ndiye niliyekiangusha niliogopa kukuambia.”
Mama yake hakumgombeza. Badala yake alimkumbatia na kusema
“Asante kwa kusema ukweli. Kuvunja kikombe si tatizo kubwa lakini kusema uongo huumiza moyo.”Neema alijifunza kwamba kusema ukweli huleta amani moyoni na hufanya watu wakuamini zaidi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment