USIFANYE MAMBO PEKE YAKO BILA KUFIKIRI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na tembo mdogo aliyeitwa Mambo. Mambo aliishi msituni pamoja na wazazi wake na wanyama wengine. Alikuwa na nguvu nyingi na alikuwa akipenda kucheza siku nzima. Lakini kulikuwa na tatizo moja Mambo hakupenda kusikiliza maelekezo ya wazazi wake.

Kila mara mama yake alimwambia “Mambo usiende mbali na msitu peke yako”

lakini Mambo hakuwa makini Alidhani anajua kila kitu.

Siku moja asubuhi Mambo aliamua kwenda mtoni peke yake kucheza majini. Njiani aliona matunda mazuri na akaacha njia salama. Ghafla aliteleza na kuanguka kwenye matope mazito. Alijaribu kutoka lakini miguu yake ilizama zaidi.

Mambo akaogopa sana. Akaanza kulia na kupiga kelele “Nisaidieni tafadhali!”

Kwa bahati nzuri Kobe na Swala walikuwa karibu. Walimwita tembo mkubwa aje kusaidia. Kwa kushirikiana walivuta na hatimaye wakamtoa Mambo kwenye matope.

Mambo alikuwa mchafu na mchovu lakini moyo wake ulijaa shukrani. Akasema kwa sauti ya upole.“Nimejifunza somo. Kuanzia leo nitasikiliza wazazi na marafiki zangu.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments