UJASIRI HUANZA MOYONI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Katika msitu mkubwa wenye miti mirefu na wanyama wa aina mbalimbali aliishi simba mdogo Alikuwa na moyo mzuri lakini alikuwa na tatizo moja kubwa aliogopa kunguruma.

Kila simba alipofika wakati wa kunguruma asubuhi alijificha nyuma ya mama yake. Alipojaribu kunguruma sauti ndogo sana ilitoka kama ya paka. Wanyama wengine walimcheka na kusema

“Simba asiyeweza kunguruma siyo simba wa kweli!” maneno hayo yalimuumiza sana. Siku moja akaamua kwenda kwa tembo mzee aliyekuwa anajulikana kwa hekima yake. Akamwambia “Nataka kuwa simba jasiri lakini ninaogopa.”

Tembo akatabasamu na kusema “Usiogope kushindwa ujasiri huanza moyoni, siyo kwenye sauti.”

Kuanzia siku hiyo alianza kujifunza ujasiri. Aliwasaidia wanyama wadogo kuvuka mto aliwalinda ndege wachanga na hakukimbia alipoona giza. Polepole hofu yake ikaanza kupungua.

Toto akajifunza kuwa simba wa kweli si yule mwenye sauti kubwa tu bali yule mwenye moyo wa ujasiri na wema.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments