TEMBO MDOGO ALIYEOGOPA MAJI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Hapo zamani katika msitu mkubwa aliishi tembo mdogo.Alikuwa na masikio makubwa, mkonga mrefu na moyo mzuri. Lakini kulikuwa na jambo moja lililomfanya awe tofauti na tembo wengine.aliogopa maji.

Kila siku tembo wote walipokwenda mtoni kuoga na kunywa maji yeye alibaki nyuma. Alikaa chini ya mti mkubwa na kuwatazama wenzake wakicheza majini.

Baada ya muda kiangazi kikubwa kilifika msituni. Mito ilianza kukauka na maji yakawa machache sana. Wanyama wote walihitaji kwenda kwenye mto mkubwa uliobaki mbali kidogo.

Mama Tembo akamwambia “Mwanangu lazima uje nasi leo. Bila maji hatuwezi kuishi.”Alitetemeka lakini akaamua kufuata kundi. Walipofika mtoni aliona maji yakitembea polepole. Hata hivyo moyo wake bado ulikuwa unaenda mbio kwa hofu.

Kobe akaanza kuingia mtoni taratibu. Maji yalifika hadi kwenye magamba yake. Tembo mdogo akaweka mguu mmoja majini. Halikuwa refu kama alivyofikiria.

Hatua kwa hatua Tembo akaingia zaidi. Alipofika katikati aligundua kitu cha kushangaza maji yalikuwa mafupi kuliko urefu wake! akapiga kelele ya furaha.

Kuanzia siku hiyo akawa tembo jasiri. Alienda mtoni kila siku. Alijifunza kuwa mara nyingi hofu ni kubwa zaidi akilini kuliko katika ukweli.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments