SUZANA NA TENDO JEMA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na mtoto mmoja aliyeitwa Suzana. Suzana alikuwa msichana mtiifu, mkarimu na mwenye upendo kwa watu wote. Kila siku alipokuwa akienda shule alipenda kuwasaidia watu njiani ambao wanakumbwa na changamoto.

Siku moja Suzana alimwona mama mmoja amebeba mzigo mzito sana. Bila kusita Suzana alimkimbilia na kumsaidia kubeba mzigo wake hadi nyumbani.

Mama yule alimshukuru sana Suzana na akamwambia


“Mwanangu Mungu akubariki kwa moyo wako mwema kwani kuna watoto wengine wapo kama wewe lakini hawawezi kufanya kitendo cha kiungwana kama wewe.”

Suzana alifurahi sana moyoni na akaendelea na safari yake kwenda shule. Shuleni mwalimu alimpongeza Suzana mbele ya wanafunzi wote kwa tabia yake njema.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments