Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Hapo zamani za kale kulikuwa na sungura mdogo aliyeitwa Kito. Kito aliishi msituni pamoja na marafiki zake ambao ni Kobe, Ndege mdogo aitwaye Pendo na Tembo.
Kito alikuwa mdogo lakini alikuwa mwerevu sana. Siku moja wanyama wa msituni walikosa chakula kwa sababu mvua haikunyesha kwa muda mrefu. Wote walikuwa na huzuni.
Kito akasema “Marafiki zangu tusikate tamaa. Tushirikiane kutafuta chakula.”
Wakaenda pamoja kutafuta matunda na mizizi. Ndege Pendo aliruka juu akaona shamba la mahindi mbali kidogo na msitu. Akawaeleza wenzake.
Kwa kushirikiana waliweza kupata chakula cha kutosha. Wote wakafurahi sana. Kobe sungura mkubwa akasema “Leo tumejifunza kuwa umoja ni nguvu.”
Tangu siku hiyo wanyama wa msituni waliishi kwa upendo na kusaidiana kila wakati.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment