Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika kijiji cha Kijani. aliishi mtoto mmoja aitwaye Simi. Simi alipenda sana kusikiliza wazee wakisimulia hadithi za kale. Alikuwa mtulivu, mtiifu na mpenda kujifunza.
Siku moja babu yake alimwambia “Kuna jiwe la busara juu ya mlima wa mbali. Mtu anayeliona na kuligusa hupata hekima ya ajabu. Lakini safari yake si rahisi.”
Simi alitamani kuliona jiwe hilo. Alisema “Nataka kupata busara ili niwasaidie watu wa kijiji chetu.”
Asubuhi iliyofuata Simi alichukua mkate, maji na fimbo ya kutembelea. Akaanza kupanda mlima mrefu. Njiani alikutana na Mzee aliyekuwa amechoka kubeba mzigo mzito.Simi alimsaidia kubeba mzigo mpaka kijijini.
Mtoto aliyepotea msituni.Simi alimwongoza hadi kwa wazazi wake.
Mbwa aliyekuwa na njaa. Abel alimpa sehemu ya mkate wake.
Kila aliyetendewa wema alimwambia “Safari yako itafanikiwa Simi.”
Hatimaye Simi alifika juu ya mlima. Aliliona jiwe kubwa liking’aa kama dhahabu. Alipoligusa sauti ilisema “Simi busara ya kweli si kuligusa jiwe
bali ni kutenda wema njiani.”
Mara moja Simi alihisi furaha moyoni. Alirudi kijijini na kuwafundisha watoto wengine kusaidiana na kuheshimu wazee.
Tangu siku hiyo kijiji cha Kijani kilijulikana kama kijiji cha amani.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment