Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Hapo zamani kulikuwa na simba mdogo aliyeitwa Lino. Lino aliishi porini pamoja na mama yake na wanyama wengine. Alikuwa jasiri lakini alikuwa na tabia ya kutokupenda kusikiliza ushauri.
Kila siku mama yake alimwambia “Lino usiende mbali peke yako. Porini kuna hatari nyingi.”
Lakini Lino hakusikia. Alijiona ana nguvu na anaweza kufanya chochote.
Siku moja Lino alimuona paa mdogo akikimbia. Bila kufikiri Lino alimfuata kwa kasi. Alikimbia sana mpaka akajikuta amepotea njia ya kurudi nyumbani. Giza lilianza kuingia na Lino akaanza kuogopa.
Akasikia sauti za fisi kwa mbali. Moyo wake ulianza kudunda kwa kasi. Akaanza kulia kwa sauti
Lino akajibu kwa huzuni “Sikusikiliza ushauri wa mama yangu.”
Tembo alimpeleka Lino hadi karibu na nyumbani. Mama yake alipoona alimkumbatia kwa furaha. Lino akaahidi “Kuanzia leo nitasikiliza ushauri na nitakuwa mwangalifu.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

.jpeg)
Post a Comment