Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Shukuru aliishi na mama yake na dada yake mdogo aitwaye Rehema. Mama yao alikuwa mfanyabiashara sokoni. Kila jioni Shukuru alimsaidia Rehema kufanya kazi za shule.
Siku moja Shukuru alicheza sana mpira na alichoka na akamwambia Rehema “Fanya mwenyewe mimi nataka kuangalia televisheni.”
Rehema alijaribu kusoma peke yake lakini hakuelewa kwasababu alizoe kusoma na kaka yake . Kesho yake shuleni alifeli maswali mengi na akarudi nyumbani analia sana.
Shukuru alihisi hatia. Akaenda kwa mama yao na kusema “Mama nilikosea kutomsaidia Rehema kwa sababu ya uzembe wangu sitorudia tena .”Mama akamwambia
“Kusaidiana katika familia huleta upendo na mafanikio na chuki huboa nyumba.”
Tangu siku hiyo Shukuru alipanga muda wa kumsaidia dada yake kila siku. Baada ya muda Rehema alianza kufanya vizuri darasani.
Shukuru akasema “Nimejifunza kuwa kuwajali wengine ni jambo la muhimu na siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment