PESA ZILIZOPOTEA NA MOYO MWAMINIFU

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na mtoto aitwaye Asha aliyekuwa akiishi na wazazi wake. Asha alikuwa mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi ya kijiji chao. Alipenda sana kusoma lakini pia alikuwa mtoto mwenye bidii nyumbani.

Kila siku baada ya kutoka shule Asha alikuwa akiwasaidia wazazi wake. Alimsaidia mama yake kuchota maji kisimani kuosha vyombo na wakati mwingine kupika chakula. Baba yake naye alimfundisha nidhamu na kusema ukweli wakati wote.

Siku moja Asha alipokuwa akirudi nyumbani kutoka shule aliona pesa barabarani shilingi elfu tano. Akaziokota na kuzishika mkononi. Asha alifurahi lakini mara moja akakumbuka maneno ya mama yake.

“Usichukue kitu kisicho chako.”Asha akasita. Angeweza kununua pipi au daftari jipya lakini dhamiri yake haikumruhusu. Akaamua kwenda moja kwa moja kwa mwalimu wake akampa pesa zile na kumweleza alipozipata.

Baada ya muda mfupi mama mmoja kijijini akaja shuleni akitafuta pesa zake.Asha alimpa yule mama pesa yake na machozi yakamtoka kwa furaha. Akamshukuru sana na kumwombea mema.

Walimu alimpongeza Asha mbele ya wanafunzi wote na kusema

“Huyu ni mfano wa kuigwa.”Asha alijisikia mwenye furaha na kujivunia maamuzi yake.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments