Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na paka mdogo aliyeitwa Kito. Kito alikuwa paka mwerevu lakini pia alikuwa mvivu kidogo. Alipenda kulala siku nzima badala ya kufanya kazi.
Siku moja mama yake alimwambia “Kito tafadhali linda chakula ili panya wasiibe.”
Kito alikubali lakini akaendelea kulala.Usiku ulipofika, panya walikuja na kula chakula chote. Kito alipoamka asubuhi, alihuzunika sana. Akaamua kubadilika.
Siku iliyofuata Kito aliweka kengele karibu na chakula. Kila panya alipokaribia kengele ililia. Kito aliweza kuwafukuza panya wote.
Mama yake akamwambia “Akili na bidii huleta mafanikio.”
Tangu siku hiyo Kito akawa paka mwenye bidii na mwenye kuwaza kabla ya kutenda.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment