NEEMA NA MSITU WA FURAHA


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Katika kijiji cha Kijani aliishi msichana mdogo aliyeitwa Neema. Neema alipenda sana kucheza karibu na msitu uliokuwa pembeni ya kijiji chao. Msitu huo ulikuwa mzuri wenye miti mingi na ndege waliokuwa wakiimba kwa furaha.

Lakini siku moja watu wa kijiji walianza kukata miti hovyo na kutupa taka ovyo. Msitu ukaanza kupoteza uzuri wake. Ndege wakakimbia na hewa ikawa chafu.

Neema alihuzunika sana. Akasema “Hatuwezi kuendelea hivi lazima tufanye jambo!”

Neema aliwaita watoto wenzake. Wakaanzisha Kikundi cha Watunzaji wa Mazingira. Kila Jumamosi walikusanya taka wakapanda miti mipya na kuwaelimisha watu kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.

Baada ya miezi michache msitu ukawa wa kijani tena. Ndege wakarudi kuimba na watu wakaanza kupumua hewa safi.

Mwenyekuti wa kijiji akasema “Neema na wenzake wametufundisha kuwa hata watoto wanaweza kuleta mabadiliko.”

Neema akatabasamu na kusema “Tukitunza mazingira tunatunza maisha yetu.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments