Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mtoto mmoja aliyeitwa Amina. Amina alikuwa mtoto mtiifu na mwenye adabu. Kila siku aliwasaidia wazazi wake kufanya kazi za nyumbani.
Siku moja alipokuwa akienda kuchota maji mtoni alimuona ndege mzuri aliyekuwa ameumia bawa. Amina alimsikitikia sana.
Amina akamchukua yule ndege kwa upole na kumpeleka nyumbani. Akamsafisha jeraha lake na kumpa chakula. Kila siku alimwangalia mpaka ndege akapona.
Baada ya siku chache ndege akawa mzima. Kabla ya kuruka alimwambia Amina
“Asante kwa wema wako.” Ghafla ndege akageuka kuwa malaika mdogo na akampa Amina zawadi ya bahati na baraka. Kisha akapotea angani.
Tangu siku hiyo Amina aliendelea kuwa mtiifu na mkarimu na familia yake ikaishi kwa furaha.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment