Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mvulana mdogo aliyeitwa Shukuru. Shukuru aliishi na wazazi wake katika kijiji kimoja. Alikuwa mtoto mnyenyekevu lakini alikuwa hapendi kusema “asante” hata akisaidiwa.
Siku moja mama yake alimpa Shukuru pesa akaenda dukani kununua sukari. Njiani mzee mmoja akamsaidia kubeba mfuko wake uliokuwa umechanika. Shukuru akachukua mfuko wake na kuondoka bila kusema chochote.
Mzee akatabasamu tu lakini Shukuru alipoendelea kutembea alianza kujisikia vibaya moyoni
Alipofika nyumbani mama yake akamuuliza “Shukuru ulimshukuru yule mzee aliyekusaidia?”
Shukuru akainama kichwa na kusema “Hapana mama.”
Mama yake akamwambia “Kushukuru ni ishara ya heshima na malezi mema.”
Shukuru akarudi haraka akamkuta yule mzee bado njiani. Akasema “Asante sana babu samahani.”
Mzee akafurahi. Shukuru akajifunza kuwa neno dogo linaweza kuleta furaha kubwa.
Tangu siku hiyo Shukuru akawa mtoto wa kusema asante kila mara.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment