Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mtoto aitwaye Baraka. Baraka alikuwa na moyo mzuri lakini hakupenda kushirikiana na watoto wenzake.
Siku moja watoto walipata mpira mmoja tu wa kuchezea. Baraka aliuchukua na kukimbia nao peke yake. Watoto wengine wakahuzunika.
Baadaye Baraka alipochoka alikaa chini peke yake. Hakukuwa na mtu wa kucheza naye. Akaona huzuni.
Akamkumbuka mama yake aliyesema “Kushirikiana huleta furaha.”
Baraka akarudi kwa watoto wengine na kusema “Samahani naomba tushirikiane.”
Watoto wakakubali wakacheza pamoja kwa furaha kubwa.
Tangu siku hiyo Baraka akawa mtoto anayependa kushirikiana.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment