Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mtoto mmoja aliyeitwa Amani. Amani alikuwa anapenda sana kusaidia watu, lakini alikuwa maskini.
Siku moja Amani alipokuwa akienda shule alimkuta mama mzee akiwa amebeba mzigo mzito. Amani akasimama akasema “Mama niruhusu nikusaidie.”
Mama mzee akafurahi sana. Walipofika nyumbani mama mzee akamshukuru Amani na kumpa tufaha moja. Amani akalichukua kwa furaha.
Kesho yake Amani alipoenda shule mwalimu aliwauliza wanafunzi “Ni nani anayejua maana ya wema?” Amani akasimama akasema.
“Wema ni kusaidia wengine bila kutarajia malipo Mwalimu akatabasamu akasema “Hiyo ndiyo jibu sahihi.”
Tangu siku hiyo Amani akajulikana shuleni na mtaani kama mtoto mwenye moyo wa upendo.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment