Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na msichana mdogo aliyeitwa Rehema. Rehema aliishi na wazazi wake mjini. Kila jioni baada ya shule alikuwa akimsaidia mama yake kufanya kazi za nyumbani hasa kufagia na kuosha vyombo.
Siku moja Rehema aliona watoto wenzake wakicheza nje. Akajisikia vibaya na kusema “Mama mbona mimnafanyai kazi kila siku na wenzangu wanacheza?”
Mama yake akamjibu kwa upole “Rehema kusaidia nyumbani ni sehemu ya kujifunza kuwajibika.”
Siku zilipita Rehema akaanza kufanya kazi zake bila kulalamika Shuleni mwalimu aliwaambia wanafunzi wafanye kazi ya vikundi. Rehema akaongoza kundi lake vizuri kwa sababu alikuwa tayari amejifunza kuwajibika nyumbani.
Mwalimu akamsifu mbele ya darasa. Rehema akatambua kuwa kazi alizokuwa akifanya nyumbani zilimjenga kuwa mtoto mzuri.
0653903872
emakulatemsafiri@gmail.com

Post a Comment