Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Palikuwa na mvulana aitwaye Besa aliyekuwa hapendi kusoma. Kila akipewa kazi ya kuandika alikuwa analalamika na muda mwingine analia kabisa.
“Kuandika kunachosha mimi sitaki jamani".Alisema Besa.
Siku moja alipokuwa njiani kwenda shule aliona kalamu ya dhahabu ikiwa imeanguka chini. Akaichukua na kuiweka mfukoni. Alipofika darasani mwalimu alisema
“Andikeni insha kuhusu ndoto zenu kisha nitazipitia za kila mmoja wenu nijue lengo lake haswa.”
Besa akatoa ile kalamu ya dhahabu akaanza kuandika. Ghafla maneno yakaanza kutoka kwa urahisi sana! Akaandika insha nzuri kuliko zote darasani.
Mwalimu akampongeza. Besa akafurahi sana. Tangu siku ile alipenda kuandika na kusoma kila siku. Lakini baadaye aligundua kuwa kalamu haikuwa na uchawi. Uchawi ulikuwa ndani yake mwenyewe ni bidii na kujiamini.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment