JUMA NA NDOTO YA NYOTA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na mvulana mmoja aliyeitwa Juma aliyeishi katika kijiji kidogo. Tangu akiwa mdogo Juma alipenda sana kutazama nyota usiku akiwa amelala juu ya mkeka nje ya nyumba yao. Alikuwa akijiuliza nyota zinatoka wapi na kwa nini zinang’aa.

Kila siku Juma alipokuwa akienda shule alisoma kwa bidii sana hasa masomo ya sayansi na hisabati. Wakati watoto wengine wakicheza mpira Juma alikuwa maktaba akisoma vitabu kuhusu anga na sayari. Wakati mwingine alichoka lakini hakukata tamaa kwa sababu alikumbuka ndoto yake.

Siku moja mwalimu wake alimwita Juma na kumwambia endelea kujitahidi. Ndoto kubwa huanza na hatua ndogo.”

Maneno yale yalimpa Juma moyo mpya. Aliendelea kusoma kwa bidii zaidi. Miaka ikapita Juma alikua na hatimaye akawa mwanaanga maarufu. Alirudi kijijini kwao kuwahamasisha watoto wengine wasikate tamaa katika masomo yao. Watoto walifurahi na wakajifunza kuwa ndoto zao zinaweza kutimia.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments