Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kupiga mswaki ni jambo muhimu sana katika maisha ya kila siku ya mtoto. Meno ni sehemu muhimu ya mwili kwa sababu hutusaidia kula na kuongea vizuri. Tunapoyatunza tunakuwa na afya bora.
Kupiga mswaki husaidia kuzuia kuoza kwa meno. Watoto wengi hupenda kula vitu vitamu kama pipi na biskuti. Vyakula hivi vikibaki kwenye meno husababisha mashimo na maumivu ya meno. Kupiga mswaki kila siku huondoa uchafu na bakteria.
Pia kupiga mswaki husaidia kuzuia harufu mbaya ya mdomo. Mtoto anayepiga mswaki vizuri huwa na pumzi safi na hujiamini anapozungumza na wenzake.Na meno safi humfanya mtoto awe na tabasamu zuri. Tabasamu huongeza ujasiri na furaha kwa mtoto.
Aidha kupiga mswaki huokoa gharama za kwenda hospitali ya meno. Meno yanapotunzwa mapema hayahitaji matibabu mengi.
Kwa hiyo watoto wanapaswa kupiga mswaki asubuhi na usiku kila siku. Wazazi nao wanapaswa kuwahamasisha watoto wao kufanya hivyo pia kupiga mswaki ni muhimu kwa afya ya meno na mwili mzima wa mtoto.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment