ETO'O APONGEZA NA KUWATAKIA KILA LAHERI MOROCCO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports

Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon, Samuel Eto’o, ameonesha moyo wa michezo na uungwana kwa kuipongeza Morocco kwa maandalizi ya mashindano ya AFCON 2025 yanayofanyika nchini humo.

Kupitia ujumbe wake, Eto’o alieleza kuridhishwa na namna wenyeji walivyojipanga kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa ya kiwango cha juu, akisisitiza kuwa juhudi za Morocco zimeipa Afrika taswira chanya kimataifa.

Alibainisha kuwa miundombinu, usalama na mapokezi ya wageni ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya taifa hilo katika kukuza soka barani.

Katika hitimisho la ujumbe wake, Eto’o aliwatakia kila la heri Simba wa Atlas, akieleza matumaini kuwa wataendelea kuonyesha soka la kuvutia na kulipa heshima taifa lao mbele ya mashabiki wao katika mechi zijazo za AFCON 2025.

Ameya sema hayo mara baada ya timu yake kuondolewa na wenyeji Morocco kwa kufungwa bao 2-0 na kuhitimisha safari Yao wakiishia robo fainali.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments