BARAKA NA SIRI YA UTIIFU

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Baraka alikuwa mvulana mdogo aliyeishi na wazazi wake Iringa. Wazazi wake walimpenda sana na walimfundisha kuwa mtoto mzuri husikiliza na kuheshimu wazazi wake.

Kila siku mama yake alimwambia “Baraka maliza kazi za shule kabla ya kwenda kucheza.”

Na baba yake alimwambia “Usichelewe kurudi nyumbani jioni.”

Baraka alikuwa mtoto mtiifu. Alimaliza kazi zake kwanza kisha akaenda kucheza. Alirudi nyumbani mapema kila siku. Wazazi wake walifurahi sana.

Siku moja marafiki zake walimwambia “Twende kuogelea mtoni mbali na kijiji.”

Lakini Baraka alikumbuka maneno ya baba yake. Akasema “Samahani siwezi kwenda mbali bila ruhusa ya wazazi wangu.”

Baadaye ilisikika kwamba watoto waliokwenda kule mtoni walipatwa na hatari kwa sababu ya maji mengi. Wazazi wa Baraka walimkumbatia wakisema “Tumefurahi kuwa ulitusikiliza. Utiifu umeokoa maisha yako.”Baraka alitabasamu na kuendelea kuwa mtoto mtiifu.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments