BAHATI HAIDUMU MILELE

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Juma alikuwa maarufu kijijini kwa kupenda sana mchezo wa karata. Kila jioni baada ya kazi za shamba alikimbilia kwenye kibanda cha mzee Musa ambako wanaume walikusanyika kucheza karata.

Mwanzoni Juma alicheza kwa kujifurahisha tu. Lakini kadri siku zilivyopit alianza kuweka dau la pesa. Aliposhinda alifurahi sana. Alipoanza kupoteza aliamini siku moja bahati ingerudi.

Siku moja Juma aliuza mbuzi wa familia bila kuwaambia wazazi wake ili apate pesa ya kucheza karata kubwa mjini. Alifika mjini na kuingia kwenye mchezo mkubwa wa usiku kucha. Alianza vizuri lakini baadaye akapoteza kila kitu pesa zote na hata simu yake.

Asubuhi ilipofika Juma alirudi nyumbani akiwa amechoka na mwenye huzuni. Wazazi wake walipogundua alichofanya, walimshauri kwa upole na kumwambia “Mchezo ni burudani lakini ukizidi hugeuka kuwa janga.”

Kuanzia siku hiyo Juma aliacha kucheza karata kwa dau. Alirudi shambani na kuanza kufanya kazi kwa bidii. Baadaye alifanikiwa kuwa mfanyabiashara mdogo na mara nyingi aliwaonya vijana wenzake.“Usiache bahati ikuendeshe. Wewe ndiye unapaswa kuendesha maisha yako.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments