ASHA NA NDOTO YA KUWA DAKTARI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Asha alikuwa msichana mdogo aliyeishi Dodoma na wazazi wake. Alipenda sana kusoma vitabu vya sayansi. Kila alipomuona daktari hospitalini moyo wake ulijaa furaha. Alisema

“Siku moja nitakuwa daktari ili niwasaidie watu wagonjwa.”

Lakini kulikuwa na changamoto. Shule yao haikuwa na vitabu vya kutosha na mara nyingine Asha alilazimika kusoma chini ya mwanga wa mshumaa. Wakati wenzake walikuwa wakicheza yeye alikuwa akisoma.


Siku ya mtihani wa taifa ilipofika Asha alikuwa na wasiwasi. Lakini alikumbuka ndoto yake. Alijitahidi sana. Matokeo yalipotoka Asha alikuwa amefaulu kwa alama za juu.

Miaka baadaye Asha alirudi kijijini kwake kama daktari. Aliwasaidia watoto na wazee kupata matibabu bora. Watu wote walimshukuru sana.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments