WAZAZI HUPENDA WATOTO WATIIFU

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na mtoto aitwaye Amina. Amina aliishi na mama yake kwenye kijiji cha kawaida si cha miujiza wala mambo ya ajabu. Kazi yao ilikuwa kulima bustani ndogo nyuma ya nyumba.

Siku moja mama yake Amina aliugua na hakuweza kwenda shambani. Amina akaamua kwenda pekee yake ingawa alikuwa mdogo. Alipalilia mboga, akamwagilia maji na kukusanya majani yaliyokauka.

Jioni mama yake akamuuliza “Nani amefanya kazi zote?”

Amina akasema “Ni mimi mama. Nilijaribu kufanya kile unafanya wewe.”

Mama yake akatabasamu na macho yakametameta kwa furaha. “Umenisaidia sana mwanangu.”

Amina akajifunza kuwa kujitahidi na kusaidia nyumbani hata kwa mambo madogo huleta furaha na heshima katika familia.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments