WASAIDIE WENGINE BILA KUTARAJIA CHOCHOTE

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na mtoto mdogo aitwaye Amani. Amani aliishi na bibi yake. Kila siku Amani alipenda kucheza kwenye msitu mdogo uliokuwa karibu na nyumbani kwao.

Siku moja Amani akiwa anatembea msituni alisikia sauti ndogo ikilia

“Tafadhali nisaidie!”

Amani alitazama huku na huku lakini hakuona mtu. Aliposogea karibu na mti mkubwa aliona mtoto mdogo amenaswa kwenye tawi lililovunjika.

“Usiogope” Amani alisema. “Nitakutoa.”

Kwa upole Amani akavunja lile tawi na kumwokoa yule mtoto. “Asante sana! Kwa kunisaidia.” alisema mtoto

Amani alimchukua yule mtoto na kumpeleka nyumbani kwao. Walipofika mama yake yule mtoto alimshukuru sana Amani na akampatia zawadi ya daftari na kalamu mbili.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872



0/Post a Comment/Comments