Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Palikuwa na tembo mdogo aliyeitwa Timo. Timo alikuwa na nguvu nyingi lakini hakuweza kufanya mambo peke yake. Alitaka kila kitu kifanyike haraka.
Siku moja Timo alitaka kuvuka mto ili afike upande wa pili kucheza. Lakini mto ulikuwa na maji mengi. Timo akajaribu kuvuka peke yake lakini akaanguka na kushindwa.
Ndipo Kima, Sungura na Ndege wakaja. Kima akasema “Tufanye kazi pamoja.”
Kima akashika mkia wa Timo, Sungura akatafuta mawe ya kuweka daraja na Ndege akawaonyesha mahali salama pa kuvuka. Kwa kushirikiana wote wakavuka salama.
Timo akafurahi sana na kusema “Asanteni marafiki. Leo nimejifunza kuwa kushirikiana ni muhimu.”
Tangu siku hiyo Timo hakudharau msaada wa wengine.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment