UKITENDA WEMA, WEMA UTAKUFATA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

 Amina alipenda sana wanyama na kila siku baada ya shule alikwenda msituni kuwasikiliza ndege wakitua na kuimba.

Siku moja alipokuwa akitembea karibu na mto alisikia. Alipofika karibu na kichaka alimkuta chura mdogo wa kijani akiwa amenasa.

Akitumia mikono yake midogo lakini yenye huruma alitenganisha matawi na kumtoa chura. Chura akamwangalia Amina kwa macho yanayometa na kusema:

“Asante! Kwa kunisaidia nitakupa zawadi ya pekee.”

Amina alishangaa. “Zawadi gani?” "Kuanzia leo kila unapotenda wema mambo mazuri yatakurudia mara mbili.”

Amina alifurahi sana lakini hakujua kama maneno hayo yangekuwa kweli.

Amina alirudi kijijini na kukuta mama mmoja akiangaika kubeba kuni nyingi. Alimsaidia bila kusita. Mama yule akamshukuru kwa tabasamu. Amina alipofika nyumbani alikuta baba yake amerudi na kikapu cha matunda maradufu kuliko kawaida. Alikumbuka maneno ya chura akatabasamu.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments