TUMBILI MCHESHI NA EMBE LA AJABU

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na tumbili mcheshi alipenda kupanda miti na kucheza na marafiki zake. Siku moja aliona embe moja kubwa sana likiangaza juu ya mti.

Embe hilo lilikuwa kubwa kuliko yote aliyowahi kuona. Liling’aa kama dhahabu.

“Aah! Hili lazima ni embe tamu kuliko yote duniani!”

Akapanda juu haraka lakini kila alipokaribia embe lilipepesa kama lina mikono likajificha nyuma ya majani. Tumbili akastaajabu

“Kwa nini embe linanikimbia?” aliuliza.

Mzee Kasuku aliyekuwa akimtazama akamwambia

“Si kila kitu kung’aa ni cha kula. Baadhi ya vitu vinahitaji akili si pupa.”

Tumbili hakusikia. Alikimbiza lile embe kuanzia juu ya tawi moja hadi lingine. Hatimaye akakanyaga tawi dhaifu likavunjika! akaanguka lakini kwa bahati nzuri aliangukia kwenye rundo la majani.

Kasuku akamkaribia akasema “Umejifunza nini kijana?”

Tumbili akavuta pumzi na kujibu “Kwamba sitakiwi kukimbilia kila kinachong’aa. Lazima nitumie akili kwanza.”

Kasuku akatabasamu “Sasa umekuwa mjanja kweli.”

Kuanzia siku hiyo alifanya kila jambo kwa utulivu na hekima si kwa pupa kama mwanzo.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments