EmakulataMsafiri
Mwanakwetukids
Katika pori la Mikumi kulikuwa na kundi la tembo waliokuwa wakiishi kwa utaratibu na nidhamu. Kundi hilo liliongozwa na tembo dume mzee aliyeitwa Mwanzo lakini kiongozi wa safari na maamuzi muhimu alikuwa tembo jike mkubwa kama ilivyo kawaida kwa tembo porini.
Mwaka mmoja kiangazi kilikuwa kikali kuliko kawaida. Mito mingi ilikauka na mashimo ya maji waliyotegemea yalikuwa yakikauka taratibu. Wanyama wengi walianza kuhama lakini tembo hawakuama bila mpango kwa sababu wanahitaji maji mengi na kulinda watoto wao wadogo.
Kiongozi wa kundi tembo jike aliyeitwa Mama Nuru alianza safari ya kutafuta maji. Aliwaongoza tembo kwa umbali mrefu akitumia kumbukumbu yake kubwa kwa sababu tembo hukumbuka njia za zamani walizopita miaka mingi iliyopita.
Baada ya siku mbili za kutembea bila kupata maji watoto wa tembo walichoka sana. Tembo wengine wakapendekeza warudi walikotoka lakini Mama Nuru aligoma kwa upole. Alisimama juu ya kichuguu akainusa hewa na akacheza kwa miguu kwa dalili kwamba alihisi kitu.
Ukweli ni kwamba tembo wana uwezo mkubwa wa kunusa na kusikia sauti za mbali hata zile zinazotokea ardhini. Mama Nuru akasikia mtetemo dhaifu chini ya ardhi ishara ya kuwa mto fulani uliokuwa karibu na kukauka bado ulikuwa na maji ardhini.
Walipofika sehemu aliyohisi hawakuona maji juu ya ardhi. Lakini Mama Nuru akaanza kuchimba kwa kutumia miguu na mkonga. Tembo wengine wakamfuata. Baada ya dakika kadhaa udongo ulianza kuwa mvuguto kisha maji yakaanza kujitokeza.
Wote wakapiga kelele za furaha kelele ambazo tembo hutumia kuonesha shukrani na amani.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment