Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Hapo zamani za kale kulikuwa na sungura mdogo aliyeitwa Toto. Toto alikuwa mcheshi sana lakini pia alikuwa mvivu. Alipenda kucheza siku nzima badala ya kufanya kazi.
Siku moja rafiki yake Kobe Kito alimwambia “Toto tukakusanye chakula mapema kabla ya mvua kunyesha.”Lakini Toto akacheka na kusema
“Ah bado kuna muda mwingi wa kucheza!”
Muda ulipita na ghafla mvua kubwa ikanyesha. Chakula kikawa kigumu kukipata. Toto akahisi njaa sana. Akaenda kwa Kobe Kito kumuomba msaada.
Kobe akamkaribisha kwa upendo na kumgawia chakula chake. Kisha akamwambia
“Kazi mapema huleta furaha baadaye.”
Toto akajifunza somo kubwa. Tangu siku hiyo akaacha uvivu na akawa sungura mwenye bidii na msaada kwa wengine.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment