Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Siku moja sungura alikuwa akitembea msituni akitafuta chakula. Alikuwa na njaa sana. Mara akakutana na mti wa ndizi wenye tunda moja tu na tunda hilo lilikuwa bivu sana na lenye harufu nzuri.
Sungura akasema “Ah! Hii ndizi itanitosha kabisa leo.”
Lakini tatizo moja likatokea ndizi ilikuwa juu sana na yeye hakuweza kuifikia. Alijaribu kuruka mara ya kwanza akakosa. Mara ya pili akakosa tena. Mara ya tatu akachoka.
Akaanza kusema “Ah hata sijui kama hii ndizi ni tamu. Labda imeoza sitaki tena!”
Lakini kwakusema hivyo moyo wake ulijua kuwa alikuwa anajidanganya kwa sababu alishindwa kuifikia.
Wakati yeye ameondoka kobe akapita. Alipoliona tunda juu akatumia ujanja wake. Aliangusha kijiti akavuta tawi taratibu na ndizi ikaanguka chini. Kobe akaila taratibu na kufurahi.
Sungura aliposikia hilo alijuta kwa kukata tamaa haraka na kujifariji kwa maneno yasiyo ya kweli.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment