Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Suzy alikuwa msichana wa darasa la tano. Aliishi na mama yake anayefanya biashara ya mboga sokoni. Baada ya shule Suzy alikuwa akimsaidia mama yake kupanga mboga na kusafisha sehemu ya biashara.
Lakini Suzy alikuwa na changamoto moja hakupenda somo la hesabu. Kila mtihani wa hesabu aliokuwa akifanya alishindwa kupata alama nzuri. Aliamini kuwa hesabu ni ngumu sana kwake.
Siku moja mwalimu wake Jamila alimwita baada ya somo.
“Suzy una uwezo mkubwa. Unachohitaji ni mazoezi na kujiamini.”
Maneno hayo yalimfanya Suzy afikirie sana. Jioni alipofika nyumbani alimwambia mama yake:
“Mama yake nataka kufanya mazoezi ya hesabu kila siku. Sitaki kukata tamaa.”
Mama yake alitabasamu kwa furaha.
Kila siku Suzy alifanya mazoezi ya maswali ya hesabu kujumlisha kutoa na maswali mengine magumu zaidi. Wakati mwingine alikuwa akikosea na kukata tamaa lakini mama yake alimtia moyo.
Ulifika wakati wa mtihani na Suzy alifanya mtihani kwa ujasiri kwa sababu alikuwa amejiandaa vizuri.Matokeo yalipotangazwa mwalimu alisema:
“Mwanafunzi aliyeongoza kwenye somo la hesabu ni… Suzy!”
Darasa zima lilishangilia. Suzy alihisi moyo wake umejaa furaha na fahari. Aliporudi nyumbani alimkumbatia mama yake kwa nguvu.
“Mama nimeweza! Mimi ndiye wa kwanza!”
Mama yake akasema kwa tabasamu “Niliamini tangu mwanzo. Ulikuwa unahitaji tu kujiamini.”
Tangu siku ile Suzy alijua kuwa jitihada na kujiamini ndizo funguo za mafanikio.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment