SIRI YA MAFANIKIO YA MTOTO MPENDA USAFI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Palikuwa na mtoto mmoja aliyeitwa Asha. Asha alipenda sana urembo na usafi. Asha hakupenda tu urembo wake binafsi bali pia alipenda mazingira safi. Alifagia uwanja wa nyumbani alipanga vitabu vyake vizuri na kuhakikisha darasa lao linakuwa safi. Alipenda pia kupamba daftari zake kwa michoro mizuri na kuandika kwa mwandiko mzuri. Wenzake walipendezwa sana na kazi zake.

Siku moja mwalimu wao alitangaza kuwa kutakuwa na shindano la darasa safi na nadhifu zaidi. Asha alifurahi sana. Aliwaongoza wenzake kusafisha darasa kupanga meza na kupamba kwa maua. Ingawa baadhi ya watoto walikuwa wavivu mwanzoni walipata moyo baada ya kuona bidii ya Asha.

Ilipofika siku ya matokeo darasa lao lilitangazwa kuwa la kwanza. Mwalimu alimpongeza Asha kwa kuwa mfano mzuri wa usafi na urembo. Wenzake walimshangilia na kuahidi kuendelea kupenda usafi kama yeye.


Tangu siku hiyo Asha aliheshimiwa sana shuleni na nyumbani.Watoto wote walianza kupenda urembo na usafi na wakatambua ni jambo jema kwani huleta afya, heshima na furaha katika maisha.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments