Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na sungura mdogo aliyeitwa Kiko. Kiko aliishi msituni pamoja na rafiki zake. kobe, ndege na Paka Madoa. Kiko alipenda kucheza sana lakini hakupenda kusikiliza ushauri.
Siku moja ndege aliwaambia “Kesho kutanyesha mvua kubwa. Tusijenge nyumba zetu karibu na mto zitabebwa na maji”.
Lakini Kiko akacheka na kusema “Mvua si kitu! Mimi nitajenga hapa hapa karibu na maji.”
Usiku ulipofika mvua kubwa ilinyesha sana. Mto ukafurika na maji yakaanza kuingia kwenye nyumba ya Kiko. Kiko akaogopa sana na kuanza kupiga kelele “Nisaidieni tafadhali!”
Rafiki zake walikimbia haraka na kumsaidia Kiko. Walimpeleka mahali salama juu ya kilima. Asubuhi Kiko aliwaangalia rafiki zake na kusema “Asanteni sana Kuanzia leo nitasikiliza ushauri wenu.”
Tangu siku hiyo Kiko akawa sungura mtiifu na rafiki mzuri.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment