Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na simba mdogo aitwaye Sefu. Sefu aliishi katika msitu mkubwa wenye miti mirefu na wanyama wengi. Ingawa alikuwa simba lakini alikuwa na tabia moja tofaut aliogopa giza.
Kila jioni jua lilipozama Sefu alikimbilia ndani ya pango la mama yake na kujifunika kwa manyoya yake. Wanyama wengine walimcheka wakisema “Simba gani anaogopa giza?”
Siku moja rafiki yake tumbili mcheshi na mwenye moyo mwema alimwambia
“Mtu shujaa sio yule asiyeogopa. Ni yule anayekubali hofu yake na bado anajaribu.”
Maneno hayo yalimfanya Sefu afikirie sana.
Usiku uliofuata msitu ulitikisika ghafla. Kulikuwa na kelele kubwa kutoka kwa pundamilia waliokuwa wanakimbia huku wakipiga makelele.
“Msaada! Mtoto wetu amekwama kwenye shimo!”
Wanyama wote walikusanyika pembeni ya shimo refu. Mtoto pundamilia alikuwa akilia bila msaada. Usiku ulikuwa na giza na hakuna aliyethubutu kushuka humo.
Sefu alijisikia moyo wake ukidunda kwa nguvu. Aliogopa lakini maneno ya rafiki yake Koko yalimjia tena.
Akasema kwa sauti ndogo lakini thabiti “Nitajaribu.”
Akatumia makucha yake kushuka taratibu ndani ya shimo. Ingawa alihisi baridi na giza lilimzunguka aliendelea kushuka mpaka akamfikia mtoto pundamilia. Kwa nguvu zake alimvuta polepole hadi juu.
Wakati walipofika nje wanyama wote walishangilia “Hongera Sefu! Wewe ni shujaa!”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment