NDEGE MDOGO NA MBEGU YA DHAHABU

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na kijiji kizuri chenye bustani kubwa. Kwenye bustani hiyo aliishi ndege mdogo aliyependa kuimba kila asubuhi.

Siku moja alipokuwa akiruka huku na kule aliona mbegu ya dhahabu ikiangaza chini ya mti. Ndege alishangaa sana.

“Hii ni mbegu ya ajabu” alisema.

Badala ya kuila ndege aliichukua na akaamua kuipanda ardhini. Kila siku aliimwagilia maji na kuiangalia ikikua.


Baada ya muda mbegu ile iligeuka kuwa mti mkubwa wa matunda. Matunda yake yalikuwa matamu sana. Ndege aliwaita wanyama na watoto wa kijiji waje wale pamoja.

Watu wote walifurahi na kumshukuru ndege mdogo kwa wema wake. Tangu siku hiyo bustani ile ikawa mahali pa furaha na upendo.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments