Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mtoto mmoja aitwaye Amina. Amina aliishi na mama yake. Mama yake alimpenda sana na alimfundisha kuwa mtii na mwenye heshima.
Siku moja mama alimwambia Amina “Usiende mtoni peke yako.” Lakini Amina hakusikiliza. Alikwenda mtoni peke yake kucheza.
Ghafla maji yakaanza kujaa na Amina akaogopa sana. Akaanza kupiga kelele kuomba msaada. Kwa bahati nzuri watu wa kijiji walimsikia na wakamwokoa.
Amina alirudi nyumbani akiwa salama. Akamwomba mama yake msamaha na akaahidi kuwa mtii siku zote.Mama yake alimchapa na kwambia kiburi si maungwana na sitaki ufanye tena hiyo tabia.
Tangu siku hiyo Amina alisikiliza ushauri wa mama yake na akaishi salama na furaha.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment