MTOTO ANAYEPENDA KUSOMA VITABU

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Bright ni mtoto wa darasa la kwanza anayependa sana kusoma vitabu. Kila siku baada ya masomo Bright hukimbia maktaba ya shule na kuchukua kitabu kipya. Wenzake wengi hupenda kucheza mpira lakini Bright hupenda kukaa chini ya mti na kusoma kwa utulivu.

Siku moja mwalimu wao alitangaza shindano la kusoma hadithi na kuisimulia mbele ya darasa. Wanafunzi wengi waliogopa lakini Bright alifurahi. Alisoma hadithi vizuri nyumbani na kuitayarisha. Siku ya shindano ilipofika Bright alisimama mbele ya darasa na kusimulia hadithi yake kwa ujasiri na furaha.

Wanafunzi wote walimshangilia na mwalimu alimpongeza kwa kusema: “Bright wewe ni mfano mzuri wa mtoto anayependa kusoma.”

Wanafunzi wengi waliamua kuanza kusoma zaidi kama Bright. Bright alifurahi kwa sababu alijua kwamba kusoma kunamjenga na kumpa maarifa mapya kila siku.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments