Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na msichana mdogo aliyeitwa Zawadi. Zawadi aliishi na familia yake katika mtaa mdogo. Kila asubuhi alisaidia kaka yake mdogo kujiandaa shule na mama yake kupika chakula cha asubuhi.
Siku moja Zawadi alipoenda shule aliona rafiki yake akilia kwa sababu alipoteza pochi yake yenye pesa za shuleni. Wanafunzi wengine walijaribu kumsaidia lakini hawakuweza kupata pochi ile. Zawadi aligundua pochi ile ilikuwa imeangukia karibu na mlango wa shule. Bila kuhesabu hatari yoyote aliruka na kurudisha pochi kwa rafiki yake.
Rafiki yake alifurahi sana na kumshukuru Zawadi. Mwalimu alimupongeza mbele ya darasa lote. Zawadi alijua kuwa kusaidia wengine na kufanya jambo sahihi kunaleta furaha kubwa zaidi kuliko kupata kitu binafsi.
Jioni aliporudi nyumbani mama yake alimpongeza na kumfundisha kuwa heshima upendo na uaminifu ni mali ya kweli. Zawadi alilala akiwa na furaha akijua amefanya jambo sahihi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment