MLANGO ULIOLIA USIKU

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na msichana mdogo aliyeitwa Neema. Neema aliishi na wazazi wake katika nyumba ya zamani iliyokuwa na mlango mmoja uliokuwa ukilia kila usiku.

Kila mtu akipita karibu na mlango huo ulitoa sauti: “Kiiiii… krrr…”

Wazazi wa Neema walimwambia “Usifungue mlango huo usiku hata ukisikia sauti.”

Lakini Neema alikuwa na moyo wa ujasiri.

Usiku mmoja wakati wote wamelala Neema alisikia kilio cha polepole kutoka mlangoni. “Nisaidie… fungua…”

Moyo wake ukapiga haraka. Polepole akasogea hadi mlangoni. Alipoufikia mlango ukaanza kutikisika!

Neema akapiga magoti na kusema “Mungu unilinde.”

Ghafla mlango ukanyamaza. Asubuhi yake walipofungua mlango walikuta upepo tu ulikuwa ukipita hakukuwa na kitu chochote!

Tangu siku hiyo Neema alijifunza kuwa sio kila sauti inahitaji kufuatwa na ushauri wa wazazi ni muhimu.Na mlango ule… haukulia tena.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments