MFAHAMU PUNDAMILIA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Pundamilia ni mnyama wa bara la Afrika anayejulikana kwa mistari yake mieusi na mieupe ambayo humsaidia kujilinda dhidi ya wanyama wakali na hata wadudu. Kila pundamilia ana mpangilio wa mistari tofauti hivyo ni rahisi kwao kutambiana.

Wanaishi kwenye savanna na maeneo yenye nyasi na hupenda kuishi kwa makundi makubwa yanayoitwa mashule. Makundi haya huwapa ulinzi na kuwasaidia kutafuta maji na chakula.

Chakula chao kikuu ni nyasi lakini pia hula majani na matawi madogo. Ni wanyama wenye nguvu na wana uwezo wa kukimbia kwa kasi kubwa wanapotishiwa.

Jike wa pundamilia hubeba mimba kwa takriban miezi 12 na huzaa mtoto mmoja. Mtoto huzaliwa akiwa na uwezo wa kutembea haraka ili kufuata kundi.

Pundamilia ni muhimu sana kwa mazingira kwa sababu husaidia kusambaza mbegu kuweka savanna kuwa na uwiano na kuwa chakula kwa wanyama walao nyama.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments