Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mbwa aliiyeishi na bibi yake. Alikuwa mcheshi, mchangamfu na alipenda sana kukimbia uwanjani.
Siku moja aliona ndege mwekundu akiruka chini akikusanya vijiti akavutiwa sana akamfuata bila kufikiria. Akaingia msituni bila kujua amekwenda mbali sana.
Baada ya ndege kutoweka akagundua kuwa amepotea. Akaanza kutembea huku na huko lakini kila alipoangalia miti ilionekana kufanana. Akaingiwa na hofu.
Akiwa amekaa chini akiwa na huzuni kobe mzee akatokezea taratibu.
Kobe akamuuliza “Mbwa mdogo mbona unalia?”
Akajibu “Nimepotea na siwezi kurudi nyumbani.”
Kobe akatabasamu “Usijali msitu huu ninautembea kila siku. Nitakuonesha njia ya kurudi kijijini.”
Wakasafiri pamoja. Mbwa alijifunza kutembea polepole, kusubiri na kusikiliza maelekezo ya kobe. Hatimaye walifika kijijini jioni.
Mbwa alipomwona bibi yake alikimbia kwa furaha
Bibi akamkumbatia “Karibu nyumbani jifunze kuwa makini na kusikiliza ushauri.”
Tangu siku hiyo hakukimbia ovyo tena na mara nyingi alimtembelea kobe kumshukuru.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment