Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Watoto mara nyingine huonesha tabia ya kukataa kula. Hali hii inaweza kuwa ya kawaida au ikawa ni ishara ya tatizo. Kuelewa kwanini watoto hukataa kula ni muhimu ili kuweza kuwasaidia kwa njia sahihi.
Sababu moja ya kawaida ni kukosa hamu ya kula. Watoto wakati mwingine wanapokuwa wachanga au wanapokua haraka hamu yao ya kula inapungua kwa muda. Pia kuota meno ni sababu nyingine inayowafanya watoto wachache kula. Maumivu ya fizi yanayohusiana na meno yanayochipuka huwatia hofu hivyo hawataki kula.
Sababu nyingine ni ugonjwa. Watoto wanaweza kukataa kula wanapokuwa na homa, mafua, maumivu ya tumbo au kuharisha. Hii ni njia ya mwili kuonesha kwamba kuna tatizo. Pia kubadilika kwa chakula au mazingira kunachangia kukataa kula.
Kwa kumalizia watoto hukataa kula kwa sababu mbalimbali kama vile kukosa hamu, kuota meno, ugonjwa na shinikizo. Wazazi wanapaswa kuwa na uvumilivu na kutumia mbinu zinazofaa kuwasaidia watoto kula vizuri. Kwa kufanya hivyo watoto wanapata lishe bora ukuaji mzuri na afya njema.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment