Adeladius Makwega-TARIME.
Wananchi wa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara wamelalamikia kutozwa shilingi 40,000/= wakati wakipima vipimo vya watoto na wanafunzi wakati kujazwa katika fomu za kujiunga na shule na taasisi za elimu kwa mwaka wa 2025/ 2026 huku wakiomba Mkuu wa Mkoa wa Mara kulitatua hili.
“Mheshimiwa ni kweli tunalipa gharama hizo kubwa, hali hii imekuwa kero na sasa kwa kuwa umefika tunaomba ulitatue mara moja.”
Haya yalikuwa ni malalamiko kutoka kwa Katibu Muenezi Kata ndugu Martias Marwa Sendi mbele ya Kanali Mtambi kikaoni.
Haya ni ya Disemba 29, 2025 wakati Kanali Mtambi alipofanya ukaguzi wa Shule ya Sekondari Bukira ambapo kulifanyika ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne ambapo ujenzi bora umefanyika.
“Malalamiko yenu nimeyapokea naagiza Uongozi wa Wilaya ya Tarime uzikague fomu hiyo za upimaji wa afya ili watoto na wanafunzi wetu waweza kupata huduma hiyo na weweze kufika shuleni kwa wakati.”
Kanali Mtambi akiongea na wananchi wa eneo hili alisema kuwa anaagiza maandalizi yote ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza yawe yamekamilika ili shule ziweze kupokea wanafunzi kwa wakati huku akiiagiza idara ya Elimu Mkoa wa Mara kufuatilia hili kwa wakati na kukamilisha mahitaji yote ikiwamo madawati.
Akilipokea agizo hili kwa mikono miwili Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Mara Mwalimu Ahidi Sinene alisema kuwa amelipokea agizo hili kwa mikono miwli na maandalizi yote yako sawa:
“Shabaha ya kuongeza walimu wapya inafanyiwa kazi maana usaili umefanyia na hivi punde walimu kadhaa wataongezwa mashuleni.”
Kanali Mtambi pia alimuagiza Afisa Mtendaji wa Kijiji hiki Bi Neema Buluba ku wa jirani zaidi na wananchi .
0717649257
Post a Comment