KILA MMOJA ANA UMUHIMU WAKE

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Hapo zamani za kale kulikuwa na msitu mzuri sana. Ndani ya msitu huo aliishi Sungura mdogo aliyekuwa mwerevu lakini mwenye kiburi. Pia aliishi Ndovu mkubwa aliyekuwa mpole na mwenye moyo mwema.

Siku moja Sungura alianza kuwacheka wanyama wengine akisema

“Nyinyi nyote ni wakubwa na wazito hamna akili kama mimi!”

Ndovu hakujibu alitabasamu tu.

Siku iliyofuata kulikuwa na mafuriko makubwa mtoni. Wanyama wadogo walishindwa kuvuka kwenda kutafuta chakula. Sungura naye alikwama akaogopa sana.


Akamwita Ndovu kwa sauti ya kuomba “Tafadhali Ndovu nisaidie!”

Ndovu alimkaribia akatengeneza daraja kwa mwili wake na kuwavusha wanyama wote salama akiwemo Sungura.

Sungura akajisikia aibu akasema “Samahani Ndovu. Leo nimejifunza kuwa nguvu na wema ni muhimu kuliko kujisifu.”

Tangu siku hiyo Sungura akawa mnyenyekevu na rafiki wa wanyama wote.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments